Watoto - Yesu ni nani?
Nick Vujicic anazungumza na watoto kuhusu Yesu ni nani. Hello, namtafuta mtu. Labda unajua yeye ni nani? Niliambiwa ninaweza kumpata katika kitabu hiki hapa. Je, unaweza kunisaidia? Mwanaume ninayemtafuta anaitwa Yesu. Sawa, nadhani Yesu hayuko katika Kitabu chenyewe, lakini nadhani atakuwa mkubwa sana hata kutoshea huko hata hivyo. Nadhani wakati watu wanasema Yesu yuko katika Biblia, kile wanachomaanisha ni Biblia inatuambia Yesu ni nini na yeye ni nani. Hapa kuna kile nilichogundua juu ya Yesu kutoka kwa Biblia, na ni ajabu sana!
Kwanza, Biblia inasema kwamba malaika alimwambia mama wa Yesu, Maria, kwamba alikuwa anaenda kupata mtoto. Maria alishangaa sana kwa sababu hakuwa na mpango wa kupata mtoto! Muda mufupi baadaye, Maria na Yosefu walikuwa wanaenda katika muji mumoja wenye kuitwa Bethlehemu. Walipofika mjini, Yesu alizaliwa, lakini si katika hospitali au hata chumba cha hoteli.
La. Yesu alizaliwa katika mazingira ya karibu na wanyama wa shamba na nyasi. Wakati Yesu alipozaliwa, jeshi lote la malaika liliwatokea wachungaji na kusema, "Nenda ukamtazame huyu mtoto mpya aliyezaliwa. Yeye ndiye mfalme, Mfalme wa wafalme, naye atawaokoa watu wote kutoka katika dhambi zao."
Watoto - Yesu ni nani? Soma Zaidi »